Watumishi wa Umma wametakiwa kufanya mazoezi ya viungo Mara moja kwa
wiki ili kujiepusha na magonjwa yasioambukiza ili kujenga watumishi
wenye afya imara kwa maendeleo ya taifa.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa magonjwa yasioambukiza (NCD)
Prof. Ayoub Magimba wakati wa kufunga mkutano Wa siku tatu wa Madaktari
na wadau wa afya ngazi ya Mkoa na wilaya katika kupata mpango mkakati wa
kujikinga na magonjwa yasioambukiza uliofanyika mkoani Morogoro.
“Katika mkutano huu wa kupata mpango mkakati wa kujikinga na magonjwa
yasioambukiza tumeazimia kua na Sera inayoelekeza watumishi wote wa
Umma wafanye mazoezi ya viungo siku moja kwa wiki ikiwa ni sehemu ya
majukumu yao”alisema Prof. Magimba.
Aidha Prof. Magimba amesema kuwa mazoezi hayo ni sehemu ya majukumu ya
watumishi wa umma ili kuwasaidia wale wanaokosa muda wa kufanya mazoezi
majumbani kwao ili kujikinga na magonjwa hayo.
Mbali na hayo Prof. Magimba amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuepuka
matumizi ya Mara kwa mara ya Sigara na vileo kwa pamoja na badala yake
wajikite kwenye mazoezi na utumiaji wa vyakula asilia.
Kwa upande wake Daktari bingwa Wa magonjwa ya ndani Dkt. Meshack
Shimwela ambaye ni mshiriki wa mkutano huo amesema kuwa watanzania
wanatakiwa kuzingatia na utekelezaji wa Sheria za barabarani ili
kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na ajali mpaka kufikia mwaka 2030.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA