Mtandao wa Wanawake Tanzania (Afnet) umetoa ripoti polisi ukidai kuna
udalali wa biashara ya ngono kwa wanafunzi wa vyuo kadhaa vya Dodoma
unaofanywa na mameneja wa hoteli zilizopo katikati ya mji
Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi wa Afnet, Sara Mwaga alipokuwa
akizungumza kuhusu maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
kwa kanda ya kati ambayo kaulimbiu yake ni "Funguka, chukua hatua,
mlinde mtoto apate elimu".
"Tumepata taarifa kuwa ziko baadhi ya hoteli hapa mjini ambazo watoto
wetu wa vyuo wamepeleka picha zao kwa mameneja anapokuja mteja anahitaji
huduma ya msichana anaonyeshwa zile picha "alisema na kuongeza
" Akichagua anapigiwa simu kama yuko wapi anapanda bodaboda ndani ya dakika 10 au 20 anamhudumia mteja anarudi ".
Alisema hayo mbele ya Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, Ernest
Kimola na maafisa wengine wa jeshi hilo na Wawakishi wa Mtandao wa
kupambana na Ukatili wa Kijinsia (Mkuki)
" Vijana wa chuoni wako katika mazingira hatarishi kwani wengi wao
huenda shule wakiwa hawana fedha kutokana na umaskini wa familia zao,
sasa mikopo inapocheleweshwa au kutopatikana kabisa huwaweka katika
mazingira hatarishi ya kushawishiwa kimapenzi.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA