Fid Q: Mwakani sintokuwa na roho nzuri

Msanii nguli wa hip hop bongo Fid Q baada ya kushuhudia EATV AWARDS mwaka huu, ameanza kujipanga kwa ajili ya mwakani na kusema kuwa hatokuwa na roho nzuri kwenye kuachia kazi.


Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Fid Q amesema mwakani amejipanga zaidi kwa kazi zake na kuachia zenye ubora zaidi, na hatokuwa na huruma.

"Nitaendelea kufanya vitu vyangu, lakini nikuweke tu wazi, mwakani sina roho nzuri, yanatoka mawe juu ya mawe, machupa juu ya machupa, kazi juu ya kazi, sina roho nzuri kwa mwakani, kwa hiyo kama kuna msanii anataka kujipanga kushindana na mimi, ajue tu kwamba mi sina roho nzuri mwakani", alisema Fid Q.

Pia Fid Q alipongeza uaandaaji wa tuzo hizo zilizofanyika tarehe 10 Desemba katika ukumbi wa Mlimani City, na kusema ameupenda mwanzo walioanza nao EATV.

Chapisha Maoni

0 Maoni