Eti kwamba kama Rais Magufuli ni jasiri au la? Ni Jasiri. Nakiri Ujasiri
hu sina.Muungwana hukiri asichokuwa nacho na kumkubali mwenye
nacho.Kwanza ule ujasiri wa kupingana na risala ya Marehemu msibani
ulikua ni uthibitisho.
-Ujasiri wa kutamka ukweli kuhusu fisadi aliyekua akiibia nchi kila
milioni 7 Kila Dakika.Unaweza kupiga hesabu hadi sasa zimeokolewa
shilingi ngapi.
-Ujasiri wa kuokoa mabilioni ya Hela kisha na bado fedha za waathirika wa majanga ya asili zikageuka kitega uchumi cha Serikali.
Ni Kweli Rais Magufuli ni Jasiri kwelikweli katika Kubana Matumizi kama
alivyofanya hili la Fedha za Kusaidia Waathirika Wa Tetemeko la Ardhi.
-Ni Ujasiri huo Pekee Uliomuwezesha Kuamua kupeleka Taa za Kuongozea
Barabarani kule Jimboni Kwake Chato wakati Miji Mikubwa kama
Dodoma,Iringa ,Morogoro ikikosa. Yeye alikuwa Waziri wa Barabara
-Ni Ujasiri huo huo uliomuwezesha kufuta ahadi ya Rais Kikwete kujengea
Nyumba waathirika wa Mafuriko kule Shinyanga.Si alishaupata Urais?
-Ni ujasiri huo uliomuwezesha kuwanunulia Chai ,Maandazi na Vitumbua
wafanyakazi wa Mghahawa pale Uwanja wa Ndege Mwanza alipotua hapo
.Alishangiliwa. Sifa ya Uwanja huu ni Kuwa Mvua zikinyesha Ndege
zinakuwa kama vile zipo Bwawani Vile na Ni Uwanja Mkubwa tu ambao ndege
kutoka Burundi,Rwanda,Kenya hutua.Ni connection Center ya Ndege za
kwenda Mikoa ya Kanda ya Ziwa...Aliamua kuwekeza kwenye Vitumbua na
vyakula pale Uwanja wa ndege na kwa ..
-Ujasiri huo ukampelekea Basi kuamua Bajeti ya Kwanza ya Serikali yake
Mabilioni ya Walipa Kodi wa Tanzania yaelekezwe kujenga Uwanja Wa Ndege
kule Kijijini kwake Chato hata kama Ndege zitakazotua pale Chato ni za
John Pombe na Rafiki yake Raila Odinga.
Si unajua Mwakani kuna Uchaguzi Kenya na Odinga atashindwa na Uhuru
Kenyatta yule aliyemtuma Lowassa aje afikishe Ujumbe Tanzania kuwa kile
Kiti kule Kenya amekikalia kwelikweli? Bila Shaka Krismasi hii au
Mwakani ndege ya Raila itatua kule kupata faraja na kujitafakari upya
kuhusu Uchaguzi Kenya
-Ujasiri huo huo utapelekea siku moja Chato kuitwa Halmashauri ya Jiji La Chato.
Ukiwa Jasiri hakuna linaloshindikana.
-Hasa ukiwa na Ujasiri unaoweza kutenga Mabilioni ya Pesa kwa ajili ya
Kukimbiza Mwenge halafu ukajifanya kutengeneza Mazingira ya kuonekana
Umeokoa bilioni 2 na ukatangaza kwa Ushujaa.
-Ujasiri wa Kumsifu Jecha na kuwashambulia Binafsi wapenda Demokrasia na haki na kuwatuhumu kuwa wana roho za kishetani.
-Ujasiri wa Aina hiihiii unaweza kumfanya hata mtu mwenye Mtoto chuo
kikuu ambae hana sifa akatukana watoto wa wenzie Vilaza kwa vile eti
anaona wamepungukiwa sifa hata kama Mwanae ni mchovu zaidi.
-Ni ujasiri huu huu unaoweza kutangaza kuahirisha safari ili
ushughulikie majanga na watu wakakuunga Mkono kisha fedha walizochanga
ukazitumia kama Chanzo cha Mapato cha Serikali hii.
-Ujasiri huu ungezaa ziara za kushtukiza kwenye matetemeko sambamba na
kuahirisha kwa Safari ya Muhimu Zambia na Mkutano wa Umoja wa
Mataifa(Ambako Kiingereza kingepaswa kutumika kwa wingi hata kwenye
Kordo maana Vifaa vya kutafsiri lugha huwa vinabaki Ukumbini)
-Ujasiri huu ukifikia hatua ya kuthubutu kuhakiki vyeti vyako kama
unavyotaka wengine wafanye utakuwa ni ujasiri endelevu(Sustainable
Bravery). Kuandelea tu Alipokomea kuwa Mfano katika Uhakiki wa silaha.
-Maana hata hilo la kutaja kupunguza mishahara ya Wengine nalo
utalifanya liende sambamba na wewe kupunguza Mshahara wako na kuweka
nyaraka hadharani kwa haraka sana ili kuwa Mfano.
-Ujasiri huu ukiambatana na kutumbua walionunua kivuko kibovu cha MV Dar
Es Salaam na Pia kutumbua waliowalipa wakandarasi hewa itakua kilele
cha Ujasiri .
Huu ujasiri alioufanya kuinyoosha nchi ya Chato sorry " Nchi ya Tanzania" bila Katiba ataupeleka katika maeneo mengine.
Kwa ujasiri huuhuu
#MagufuliHakikiPhDyako
#Magufulideclareyourpaytubes
A Luta Continua,Victory Ascerta...
Ben Saanane
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA