MONICA: Mwanamke mnene mwenye malengo ya kunenepa zaidi

Kutana na Monica Riley, dada mwenye umri wa miaka 27 ambaye amejaaliwa unene wa kutosha lakini bado anahitaji kunenepa zaidi ili afikie lengo la kuwa mwanamke mnene kuliko wote duniani.


Monica ameweka bayana kuwa lengo lake ni kunenepa hadi ashindwe kujisogeza ili awe kama Malkia, yaani afanyiwe kila kitu.

Bwana'ake, Sid Riley ambaye ni kijana wa miaka 25, ndiye msaada wake mkubwa haswa kwenye masuala ya mapishi na kumlisha. Sid hana tatizo na suala la baby wake Monica kwani yuko nae sambamba.

Mama yake Monica alishawahi mtahadharisha bintiye kuhusu unene huo kuwa utamsababishia maradhi na hata kifo, lakini Monica mwenyewe ameonyesha kutojali na anataka aachwe aishi apendavyo.

Kwa sasa, Moni na Sid wanafanya jitihada ya kupata mtoto licha ya kujaribu mara kadhaa na mimba zote kuharibika. Na kuhusu kumlea, amesema atatafuta kijakazi wa kumsaidia kulea.

Kuna mengi kuhusu Monica ila hayo ni muhtasari tu. Malengo yake ya msingi kwa sasa ni kufikia uzito wa Kilo 1000.

Chapisha Maoni

0 Maoni