Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila anazidi kupokea shinikizo kimataifa kutokana na hatua ya kukataa kuachia maamlaka baada ya muhula wake wa kikatiba kukamilika jumatatu.
Ufaransa imesema itatuma ombi kwa umoja wa ulaya la kumwekea vikwazo iwapo ataendelea kushikilia maamlaka.
Ujerumani imehairisha majadiliano ya kuipa DR Congo msaada wa miradi ya maendeleo.
Inaripotiwa kwamba utulivu umerejea nchini humo baada ya kushuhudiwa machafuko Jumatano, ambapo kulingana na Umoja wa Mataifa, takriban watu 20 waliuwawa.
Uchaguzi mkuu ulioratibiwa kufanyika mwaka huu, uliharishwa hadi mwaka 2018
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA