Kanali Mjengwa alia na demokrasia

Mbarali. Mkuu wa wilaya mstaafu, Kanali Edmund Mjengwa amesikitishwa kuminywa demokrasia nchini.


Kanali Mjengwa amesema hafurahishwi na namna upinzani unavyominywa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani.

Amesema mfumo wa demokrasia ya vyama vingi nchini uliridhiwa na Serikali ya CCM yenyewe miaka ya 1990, hivyo haiwezekani Serikali hiyohiyo inayoongozwa na CCM ikasema siasa hadi mwaka 2020.

“Mimi ni mwanaCCM haswa, niliyelelewa na kukulia ndani ya CCM tangu tunapata uhuru mwaka 1961, hivyo ninakifahamu vyema kabisa chama changu na hapa najiuliza hivi chama changu ndicho kilichoiamuru Serikali iminye upinzani au ni Serikali yenyewe? Nasema hivi, upinzani hautendewi haki kabisa,” amesema.

Chapisha Maoni

0 Maoni