SERIKALI INATARAJIA KUAJIRI WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI KWA SHULE ZA SEKONDARI NCHINI.
AJIRA HII NI KWA WALIMU WA DIPLOMA NA DIGRII WALIOHITIMU MAFUNZO YA SAYANSI NA HISABATI MWAKA 2015.
WAHITIMU HAO WANATAKIWA KUWASILISHA NAKALA ZA VYETI VYAO VYA ELIMU SEKONDARI (KIDATO CHA NNE NA SITA) NA TAALUMA YA UALIMU KWA AJILI YA UHAKIKI.
NAKALA HIZO ZIWASILISHWE KUPITIA EMAIL info@moe.go.tz KUANZIA LEO HADI TAREHE 16/12/2016(IJUMAA).
YEYOTE AMBAYE VYETI VYAKE HAVITAHAKIKIWA HATAFIKIRIWA KATIKA UAJIRI.
TANGAZO HILI LINAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA NACTE,TCU,NECTA,MOE NA TAMISEMI.
imetolewa na:
Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA