Akizungumza na wakazi wa kata ya Kwamagome iliyopo wilayani Handeni wakati alipokwenda kukagua ujenzi wa zahanati ya kata hiyo, waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, watoto na wazee Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema serikali haiwezi kukubali kusikia hospitali za wilaya hakuna dawa na akatoa mfano kuwa hospitali ya wilaya ya Handeni katika bajeti ya mwaka jana wamepewa milioni 53 na mwaka huu wameiongezea hadi kufikia mil 110 hivyo anashangazwa kusikia baadhi ya hospitali hazina dawa.
Hatua hiyo inafuatia baadhi ya wasaidizi wa wagonjwa waliokutwa katika hospitali ya wilaya ya Handeni, kulalamikia tatizo la kukosekana kwa dawa hospitali ya wilaya ya Handeni na kuiomba serikali kuingilia kati kwa sababu wanalazimika kwenda kununua dawa katika hospitali za watumishi wa afya baada ya kuelezwa kuwa hoapitali hakuna.
Kufuatia hatua hiyo mkuu wa wilaya ya Handeni Godwini Gondwe amesema wilaya yake wameanzisha kampeni ya kuwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii,inayomshinikiza kiongozi wa familia kuuza kuku mmoja ili aweze kujiunga na mfuko huo.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA