Baada ya kuahirishwa kwa mchezo wa Europa League kati ya Sassuolo ya Italia iliyokuwaicheze na KRC Genk ya Ubelgiji inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta kwa sababu ya hali ya hewa ya uwanja kuwa na ukungu kiasi wachezaji kutoweza kuonana vizuri jana December 8.
Mchana wa December 9 2016 ulichezwa mchezo huo wa mwisho wa Kundi F katika uwanja wa Mapei Italia, KRC Genk imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli yakifungwa na Bryan Heynen dakika ya 58 baada ya kupewa pasi na Samatta na goli la pili lilifungwa na Leandro Trossard dakika ya 81.
Matokeo hayo yamewafanya KRC Genk kuongoza Kundi F kwa kufikisha jumla ya point 12 wakifuatiwa na Athletic Bilbao ya Hispania wenye point 10, KRC Genk na Athletic Bilbao wamefanikiwa kutinga hatua ya 32 bora ya michuano hiyo, bado haijajulikana na atacheza na nani hadi droo itakapochezeshwa.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA