Ushindi wa tuzo ya Muigizaji bora wa kike wa Tuzo za EATV 2016 kumemtoa machozi Chuchu Hansy na kumkumbusha mambo mengi aliyopitia kwenye maisha yake.
Muigizaji huyo ambaye hakuwepo kwenye usiku huo wa tuzo na kuwakilishwa na meneja wake, ametoa ya moyoni kupitia Instagram kwa kusema ushindi huo umemfanya akumbuke maneno aliyokuwa akipewa na mama yake katika kipindi cha ukuaji wake.
“Naamini kuna uwepo wangu kwa kila hatua tupigayo, ama hakika usitamalaki ya moyoni kwa kuyadhihaki ya machoni. Hii imenipa funzo zaidi ya lile alilonipa mama nikiwa na vunja ungo,” alisema Chuchu. “Mama aliniambia heshimu watu bila kuwa dhihaki kwa makundi,ama kuwa bagua kwa rika,”
“Niwashukuru wote mlio nipigia kura amahakika mme tenda vema,likini mimi sio bora kuliko wenzangu ila nadhani kwa wino wakura zenu ulistahili niwe BEST ACTRESS, niwashukuru zaidi na zaidi, nikiandika maneno haya machozi yananitoka lakini hii yote ni heshima mlio nivika NENO LA KALE NI ASANTE,” aliongeza.
Katika kipengele hicho cha muigizaji bora Chuchu alikuwa anachuana na Khadija Ally, Kajala Masanja, Rachael Bitulo, pamoja na Frida.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA