Wizara ya Mambo ya Nje kupunguza wafanyakazi katika Balozi zake

Katibu mkuu wizara ya mambo ya nje, Dr. Aziz Mlima
Katika kuhakikisha kuwa serikali inabana matumizi ya fedha, Wizara ya Mambo 
ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inatarajia kupunguza wafanyakazi katika Balozi zake na kuweka wafanyakazi wapya.


Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk. Aziz Mlima katika mahojiano na TBC1 ambapo alisema kuwa katika kupanua wigo huo wamewaondoa wafanyakazi kwenye Balozi 35 na ofisi mbili za uwakilishi zilizopo nchi mbalimbali.

Ameongeza kuwa wameona ni vyema kuwabadilisha wafanyakazi waliokuwepo na kuweka wapya ambao watakuwa wachache na wenye uwezo wa kufanya kazi kama invyotakiwa.

Akizungumzia lengo la Kupunguza wafanyakazi amesema ni kuongeza uwakilishi mzuri, kuwa na watu wachache kwa kuwa miongoni mwa majukumu ya Balozi za Tanzania ni pamoja na kutangaza fursa za utalii na vivutio vilivyopo nchini ili kuongeza watalii kutoka nje.

Chapisha Maoni

0 Maoni