JPM afanya mazungumzo na billionea Dangote, amhakikishia hakuna tatizo, watu binafsi walitaka kujinufaisha.

Rais Magufuli leo Desemba 10 amekutana na kufanya mazungumzo na mmiliki wa Kiwanda cha Dangote Mtwara, Bilionea namba moja Afrika, Alhaji Aliko Dangote.


Rais Magufuli baada ya kufanya mazungumzo na Dangote amesema hapakuwa na tatizo bali watu tu waliotaka kujinufaisha kupitia mradi huo kiujanjaujanja.

Rais amemtaka Dangote kununua gesi moja kwa moja toka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya kutumia watu wengine.

Amemhakikishia Dangote serikali itaendeleza mazingira mazuri kwa Wawekezaji ili kutimiza lengo la Tanzania ya Viwanda.

Chapisha Maoni

0 Maoni