Marufuku ya matumizi ya adhana{ Wito
kwa Waislamu kuhudhuria maombi} katika tarafa moja ya mji wa Kigali
nchini Rwanda imepingwa vikali na baadhi ya Waislamu jijini humo.
Utawala
katika tarafa ya Nyarugenge kunakopatikana jamii kubwa ya Waislam
nchini humo umebainisha kuwa kumekuwepo muafaka wa kubadili mbinu za
kuwaita waumini bila ya matumizi ya njia hiyo ambayo inatajwa kuwasumbua
wananchi.
Kulingana na mwandishi wetu mjini Kigali John Gakuba
wito huo wa Waislamu kuhudhuria maombi umetajwa kuwa kero miongoni mwa
wananchi.
Tayari mkataba wa kuhakikisha kuwa mwafaka huo unaheshimiwa umetiwa saini kati ya viongozi wa msikiti na utawala wa eneo hilo.
Wito huo wa mamombi miongoni mwa jamii za Waislamu kote duniani hutumia vipaza sauti na hufanyika mara tano kwa siku.
Licha
ya utawala wa eneo hilo kudai kwamba kumekuwa na mwafaka kutoka pande
zote mbili baadhi ya Waislamu waliohojiwa wametoa hisia tofauti.
Kulingana
na katibu mtendaji wa tarafa hiyo ya Nyarugenge, amri hiyo iliagizwa
yapata miaka maiwili iliopita lakini ikapuuziliwa mbali.
''Pengine
wakati ule sababu ambazo watu hawakupokea vyema ujumbe ilikuwa hakuwa
umeelezewa sawa sawa ,lakini leo baadhi ya makanisa yalilazimika kufunga
milango baada ya kushindwa kutimiza kanuni za ujenzi huku misikiti
yenye vipaza sauti na makanisa yenye kengele tukiyataka kutotumia
mtindo huo. Mtu aliye lala akiishi jirani na kengele hiyo inampigia
kelele. Kwa hiyo ni uamzi unaohusu pande zote nna ni matarajio yetu kuwa
hakuna aliyenyimwa haki.''
Naye mshauri wa Mufti wa Rwanda shekh
Mbarushimana Suleinam alisema kuwa hatua hii ya kuzuiliwa kwa matumizi
ya adhana misikiti inafuatia operesheni inayoendela ya kufungwa kwa
makanisa na vigango Zaidi ya mia saba ambavyo viliripotiwa kuwa
havijatimiza kanuni za ujenzi na amri ilitolewa kwanza kutimiza matakwa
ili zipewe tena idhini ya kufanya kazi.
CREDIT: BBC SWAHILI
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA