DC Polepole: Mange ni kipande cha chumvi kwenye bahari

Polepole ameanza kazi kwa kasi kubwa baada ya kuamua kuanza na Mange Kimambi na kumfananisha na kipande cha chumvi kwenye bahari.Polepole amesema hayo alipokuwa akiongea na gazeti la Mzalendo mtandaoni (online) ofisini kwake baada ya kampeni ya kuchoma kadi za CCM inayoendeshwa na Mange Kimambi kushika kasi kila kukicha mitandaoni.

Amedai Mange ni kipande cha chumvi baharini,madhara yake ni madogo, huku akienda mbali zaidi na kudai hata kama ni chumvi basi ladha yake imepungua kutokana na historia aliyopitia Mange katika mahusiano yake,familia yake na suala lake la uchumi.
Pia Polepole alisisitiza kadi zinazoonekana kuchomwa moto sio kadi za CCM bali karatasi za kijani zinazofanana na kadi za CCM.      

Chapisha Maoni

0 Maoni