Mbunge wa Solwa (CCM) Ahmed Salum, amedai Serikali imeweka sera mbovu
kuhusiana na bandari kwa kuweka kodi ambazo zimewakimbiza
wafanyabiashara pia amesema TRA hawakusanyi kodi ila wanakusanya
malimbikizi ya nyuma na baada ya muda malimbikizi hayo yataisha na
ukusanyaji utarudi bilioni 850 kama Kikwete alivyoacha.
Amesema washauri wa Magufuli hawamuambii ukweli kutokana na woga
Amesema sSngle Custom Territory na VAT kwenye transit goods
zimewakimbiza wafanyabiashara na wafanyabiashara wamehamia bandari za
nchi za jirani
Leo hii waziri wa fedha ameacha kodi za matrilioni bandarini wanaenda
kukabana bodaboda na trafiki wanakusanya faini barabarani kama vita.
alisema hivi sasa kuna tatizo la mzunguko wa fedha katika jamii, huku
akishangazwa na kauli ya Waziri Mpango ya uchumi kuimarika.
Alisema anashangazwa na taarifa ya kuimarika uchumi, japo bado kuna
matatizo ya uchumi, ikiwamo upande wa wawekezaji wanaokuja nchini.
Mbunge huyo alisema hakuna kituo kimoja kwa ajili ya kuhakikisha
wawekezaji hawasumbuliwi, lakini bado kuna tatizo Kituo cha Uwekezaji
(TIC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao hukaa na nyaraka muda
mrefu bila kufanya uamuzi.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA