Background (kwa kifupi)
Mh Othman alikuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Uandishi wa Bunge la
Katiba (a.k.a Bunge la Sitta (rip)). Tarehe 1 Oktoba 2014 aliibua
mshangao mkubwa baada ya kupiga kura ya kukataa baadhi ya vipengele vya
Rasimu ya Katiba ambayo tayari UKAWA walikuwa wameishaisusia baada ya
kuchakachuliwa kwa Rasimu ya Katiba ya Wananchi
(a.k.a Rasimu ya
Warioba).
Baada ya uamuzi wake wa kujitoa kwenye Bunge la Katiba, Mh Othman
anasema Rais Shein alimuita na kumtaka ajiuzulu, lakini akakataa
akimweleza kuwa kwa sababu yeye (Rais) ndiye aliyemteua, na yeye
(Othman) anaona hajatenda kosa lolote, basi Rais atengue uteuzi ule
mwenyewe kama ataona inafaa. The rest is history.
Mh Othman afafanua kwa nini alipiga kura ya kukataa vipengele kadhaa kwenye Rasimu ya Katiba:
- Zanzibar haikwenda kwenye Bunge la Katiba ikiwa na msimamo wake na kwamba Dk Shein alishindwa kutetea visiwa hivyo.
- wajumbe kutoka Zanzibar hawakuwahi kukutana na kujadiliana kwa pamoja
jinsi ya kutetea masilahi yao, licha ya Rais Shein kushauriwa
kuwakutanisha. Hivyo kila mtu alikwenda kivyake kwenye Bunge la Katiba.
Walikwenda na misimamo yao ya vyama. "kwa bahati mbaya mimi sifungwi na
misimamo ya vyama hivyo viwili. Watu waliomba si mara moja si mara mbili
kwa Rais kwamba tukae. Makamu wa Kwanza (wakati huo Maalim Seif Sharif
Hamad) alikwenda kumuomba, mawaziri walikwenda kumuomba kwamba tukae
tujadili masilahi ya Zanzibar, lakini hatukukutana,” alisema.
- kilichomkera zaidi Mh Othman ni kuwekwa kwenye Kamati ya Uandishi wa
Katiba ambayo alisema ilipewa maelekezo ya nini cha kuandika. “Nakumbuka
kanuni ya 35 inasema kazi ya Kamati ya Uandishi ni kukusanya yale
yaliyotoka kwenye Kamati za Bunge. Sasa ugomvi wangu ulikuwa ni mambo
yaliyojadiliwa kwenye hizo kamati, yalitokana na waraka wa CCM uliotoa
maelekezo ya mambo yaliyotakiwa kuandaliwa,” alisema
- anaendelea... “kwanza nilikuwa sikubaliani na mambo mengi
yaliyojadiliwa kwenye hizo kamati. Pili, kwenye kuandaa hiyo ripoti ya
chama, mimi sikushiriki ingawa kwa upande mwingine, Mwanasheria Mkuu wa
wakati huo na wanasheria wengine walishirikishwa, akiwemo Jaji Fredrick
Werema”
- sababu nyingine ni wajumbe walioteuliwa kuandika Katiba
Inayopendekezwa kuandaliwa kila kitu na mchakato kukosa misingi ya
uandishi. anasema “kwa hiyo sikutaka jina langu liwemo kwenye rasimu
ambayo sikuiandaa, ndiyo maana nikajiondoa. Uzuri ni kwamba sikuteuliwa
kwenye ile kamati kama Mwanasheria Mkuu (wa Zanzibar), bali niliteuliwa
kama Othman, mjumbe wa Bunge la Katiba,” alisema.
- Mh Othman anaongezea kusema kabla ya kujitoa Kamati ya Uandishi,
wajumbe wenzake kutoka Zanzibar, wakiwamo mawaziri wa Zanzibar
walikutana na kuweka msimamo wa mambo manane kati ya 17 waliyotaka
yaingizwe kwenye Katiba hiyo, lakini baadaye yalikataliwa.
- Baadhi ya mambo hayo muhimu ni:
(a) uwezo wa Rais wa Muungano kugawa mipaka ya Zanzibar, akisema
walitaka Rais wa Zanzibar awe na mamlaka hayo kwa mujibu wa Katiba ya
mwaka 1982.
(b) Katiba ya Jamhuri ya Muungano isiguse mambo yasiyo ya Muungano ambayo yatakuwa chini ya Katiba ya Zanzibar.
(c) suala la ardhi ambalo awali lilikuwa chini ya Muungano, akisema lilipaswa kuwa chini ya Zanzibar
(d) jinsi ya kumpata Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kutumia wingi wa
kura, jambo ambalo alisema haliwezekani, akipendekeza Rais apate japo
asilimia 20 ya kura za Wazanzibari ndipo ahesabike kuwa mshindi. Mh
Othman ametolea mfano Kenya na Marekani ambako minority (geographically)
wanapewa appropriate leverage jinsi ya kumchagua mkuu wa nchi
(e) mambo mengine aliyataja kuwa kuwa ni mfumo wa kodi, suala la kupiga
kura ndani ya Bunge na kubadilisha mfumo wa Serikali. Alitaja pia kero
ya wabunge wa Zanzibar kutokuwa na nguvu ya uamuzi katika Bunge la
Jamhuri ya Muungano, akisema ndiyo kubwa aliyoipigania
Mh Othman anaonyesha mshangao “sisi tunajiuliza, wabunge wa Zanzibar
kama hawana sauti kwenye mambo ya Muungano, wanakwenda kufanya nini
pale? Kuna haja ya kuwa na wabunge wa Zanzibar kama hawana sauti?"
Mh Othman anamalizia kwa kusema waliyajadili mambo hayo wakiwa na mawaziri wa Zanzibar, lakini baadaye wakabadilika.
Anaongeza hapa “Baadaye wakasema jamani tumeshakaa hapa tumekula pesa ya
watu, tupitisheni tu kwa sababu hayataingia kwenye Rasimu ya Katiba.
Waliponifuata nilikataa kwa sababu kumbukumbu inayobaki hapo ni Katiba
Inayopendekezwa.”
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA