Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe amesema anaamini Edward Lowassa
hakuenguliwa kwa haki na CCM katika mchakato wa kumpata mgombea urais wa
chama hicho, na kwamba waziri mkuu huyo wa zamani si pekee ambaye
amekumbana na uonevu kama huo.
Bashe, ambaye ameingia bungeni kwa mara ya kwanza katika Uchaguzi Mkuu
wa mwaka jana akipeperusha bendera ya CCM, pia amesema kashfa zote
zinazoikumba Serikali hutengenezewa suluhisho kwa malengo fulani na si
kutafuta muafaka wa haki.
Kiongozi huyo wa zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM alisema hayo katika
mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Bashe, ambaye alikuwa kambi ya Lowassa wakati wa mchakato wa kumpata
mgombea urais wa CCM, alisema ingawa hana uhusiano tena wa kisiasa na
kada huyo, anaona tukio lake kuwa ni historia ya kutotendea haki
wanachama wengi wa CCM. “Si Lowassa pekee, wako wengi,” alisema Bashe
katika mahojiano hayo.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA