KIMEI: CRDB hatujapata hasara, watu wanazusha

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Charles Kimei amesema benki yao haijapata hasara ila wametengeneza faida ya bilioni 63 robo tatu ya mwaka kutoka January hadi Septemba.

Amesema kilichofanyika ni wameweka sehemu ya faida iliyopatikana kama reserve kwa ajii ya wadaiwa wake ili kujiandaa mapema na kama mikopo hiyo itarudishwa basi itarudishwa kama faida na watu wakashindwa kutafsiri

Pia benki hiyo ina mikakati ya kuongeza amana(deposits) za benki kutoka kwa wateja wadogo na wakubwa na hawezi kujiua wenyewe kwa kupunguza matawi.

Amesema mwaka jana pekee wamefungua matawi 70 na kuajiri watu 450 jamboambalo benki nyingi nchini haziwezi kufikia.

Mwaka huu wamepanga kufungua matawi 75 na kuajiri wafanyakazi 460

==============
CRDB hawajapata actual hasara lakini wameona kuna hasara kubwa inakuja ndio maana wakaweka hiyo provision kwa ajili ya doubtful debts, hii ni prediction kuwa kuna hali ngumu inakuja ya watu kushindwa kurejesha mikopo yao.

Chapisha Maoni

0 Maoni