Wilaya ya rombo ni wilaya iliompakani mwa Kenya na Tanzania iliyo na
hali ya hewa nzuri huku ikizungukwa na msitu mnene wa mlima kilimanjaro
zao kuu la kibiashara ni ndizi na kahawa japo kahawa imepoteza thamani.
Ni wilaya ilio karibu sana na jiji la Nairobi ni takribani masaa matatu
au manne hivi kutoka wilaya ya rombo hadi Jiji la nairobi . Wakazi wake
wengi hufanya biashara jiji la Nairobi kuliko miji ya Tanzania . Wakazi
wake ni wa kipato cha kati sio maskini sana na wala sio matajiri sana .
Wilaya ya Rombo ina miundombinu ya barabara nzuri sana.
Wananchi wake wengi wanatumia bidhaa kutoka nchini Kenya kutokana na
kukosekana kwa vyombo vya habari vya kutangaza bidhaa za Tanzania Jambo
la kusikitisha wilaya hii hamna station ya redio ya Tanzania inayoshika
hata moja kwa hiyo wakazi wengi wa Rombo wanasikiliza sana station
redio za kenya .
Hili limefanya wilaya hii kutojulikana vizuri na watu kutokuwepo na
uelewa mpana wa mambo yanayoendelea nchini mwao. Wilaya ya Rombo
japokuwa ni wilaya kongwe hapa nchini haina hospitali ya wilaya.
Njoo sasa kwenye majengo ya mahakama, kituo cha polisi cha wilaya pamoja
na Magereza ya wilaya hazina hadhi kabisa ni zaidi ya magofu . Wilaya
ya Rombo ni wilaya iliosahulika kama iko Tanzania japokuwa ina
wafanyabiashara wakubwa Tanzania na kenya.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA