MAKONDA ATINGA UWANJA WA FISI, TANDALE KATIKA KATA YA MANZESE, ASHUHUDIA MADANGURO TELE YA BIASHARA YA UKAHABA, ASEMA SERIKALI ITAYAVUNJA

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akibisha hodi kwenye mlango mmoja katika banda linalodaiwa kutumiwa kwa biashara ya ukahaba, katika eneo maarufu kwa jina la Uwanja wa Fisi, lililopo, Tandale Kata ya Manzese, akiwa katika siku ya tisa ya ziara yake
mkoani humo leo. Wapili ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Salum Hapi na Kamanda wa  Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro. 

Akiwa katika eneo hilo baada ya kukatiza vichochoro kadhaa, alifika eneo la klabu cha pombe za kienyeji, na kuzungumza na mmoja wa wateja waliokuwa wakinywa hapo..

"Hii achana nayo kabisa ni moto wa kuotea mbali. Hebu niikate kidogo uone", Mzee aliyejitaja kwa jina la Mandela, alimtambia Makonda huku akipiga funda la pomne hiyo ya kienyeji hali inayoonyesha kuwa hakuwa akifahamu kuwa anayezungumza naye ni Mkuu wa mkoa.

Baadaye alienda eneo lenye vibanda vya chumba kimoja kimoja, amabavyo inaelezwa kuwa ni madanguro ambayo hutumika kufanyika biashara ya ukahaba hadi kwa wasichana wenye umri mdogo.

Hata hivyo kila mlango aliojaribu kugonga Makonda, ulikuwa umefungwa na hakuna aliyeitika hodi yake.

" Hawa wakijua watu wa serikali wanakuja hapa basi hufunga biashara zote. sasa na hapa wamefunga, si rahisi kumpata mtu" Kijana mmoja mwenyeji wa eneo hilo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Shuleya Msingi Tandale Makonda alisema, serikali inafanya mipango ya kupata wawekezaji ili kununua eneo hilo la Uwanja wa Fisi na kuwalipa fidia wakazi wa eneo hilo ili vibanda vyote vivunjwe na kujengwa vitegauchumi. badala ya kuliacha eneo hilo liharibu maisha ya vijana.

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akibisha hodi kwenye mlango mmoja katika banda linalodaiwa kutumiwa kwa biashara ya ukahaba, katika eneo maarufu kwa jina la Uwanja wa Fisi, lililopo, Tandale Kata ya Manzese, akiwa katika siku ya tisa ya ziara yake mkoani humo leo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Salum Hapi. Ebdelea kuona taswira mbalimbali katika picha kama zilivyopigwa na Blogger na Msimamizi Mkuu wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, ambaye ameambatana na Makonda kwenye ziara hiyo.
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, akimsaidia Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kubisha hodi kwenye mlango mmoja katika banda linalodaiwa kutumiwa kwa biashara ya ukahaba, katika eneo maarufu kwa jina la Uwanja wa Fisi, lililopo, Tandale Kata ya Manzese. 
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikabidhiwa bia na mhudumo wa baa pekee aliyoikuta ikiwa wazi, wakati wa ziara hiyo katika eneo la Uwanja wa Fisi
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiichunguza kwa makini bia hiyo, ili kuthibitisha kama muda wake wa matumizi bado haujapita. Makonda alisema, kuna taarifa kwamba wafanya biashara za vileo katika Uwanja wa Fisi wamekuwa wakiuza viwaji hadi vilivyokwisha mda wake wa matumizi.
 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Salum Hapi, akimpatia maelezo Makonda baada ya kufika eneo la Uwanja wa Fisi, Tandale, kata ya Manzese.


 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wateja wa pombe za kienyeji kwenye kilabu cha pombe hizo kilichopo Uwanja wa Fisi, apofanya ziara katika eneo hilo leo
 Mteja wa pombe za kienyeji anayejiita Mandela, akikata kiu mbele ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na kutojua kuwa alikuwa amekaa na Kiongozi
 Kijana huyu ni miongoni mwa vijana wanaodaiwa kuwa wateja ambao hukesha Uwanja wa Fisi, naye alikuwepo leo

Chapisha Maoni

0 Maoni