November 22 2016 ziara ya Mkuu wa mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul
Makonda iliendelea kwenye viwanja vya Zakhem Mbagala, lengo ikiwa ni
kutafuta majibu ya kero za wananchi, hapa alikutana na kero ya mwananchi
ambaye alivunjiwa nyumba yake toka mwaka 1988 na mwakilishi wa idara ya
ardhi kutoka manispaa ya Temeke alipopewa nafasi ya kujibu hakutoa
majibu yaliyomridhhisha RC Makonda.
‘Ninyi watu wa ardhi ndio maana mnaona viongozi kama vichaa vile, hivi
ujanja mtaacha lini? mzee kama huyo tangu mmvunjie 1988 miaka yote hiyo
mpaka leo mzee wa watu bado ana maumivu kwenye moyo wake, mnasema mzee
leta vithibitisho, mnamtengeneza mahali ambapo hawezi kuwa na nyaraka
mnazozitaka ninyi ili ashindwe, mnajua katika watu ambao hamtaingia
mbinguni ni watu wa ardhi’- RC Makonda
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA