Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua za vuli zinazoendelea
kunyesha nchini ni mvua ambazo kama wananchi hawatachukua tahadhari za
haraka zinaweza kuleta madhara makubwa.
Hayo yamesemwa na Meneja Kitengo Kikuu cha Utabiri cha Mamlaka hiyo, Bw.
Samwel Mbuya wakati akitoa ufafanuzi wa mvua zinazoendelea kunyesha
nchini na kusababisha madhara kwa baadhi ya mikoa.
Amesema mabadiliko ya hali ya hewa kwa sasa yanatokana na kuwepo kwa
msimu unaotawaliwa na uwepo wa LANINA ambayo ni ongezeko la hali ya
baridi katika eneo la Ikweta ya Bahari ya Pacifiki.
Amesema bado matarajio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa na upepo
vitaendelea kuwepo katika msimu huu mpaka mwezi Desemba na mabadiliko
kidogo yatajitokeza kwa baadhi ya mikoa ambapo mvua zitanyesha kwa
wastani.
Akizungumzia hali ya joto amesema itaongezeka kwa baadhi ya mikoa hasa ya Dar es Salaam itaendelea kuwepo kwa kipindi kirefu.
Kuhusu watumiaji wa vyombo vya bahari amewatahadharisha kuzingatia
taarifa za hali ya hewa ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea
kama taadhari hizo hazitazingatiwa.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA