Watumishi wapya walioajiriwa mwezi June 2016 kisha kusainishwa mikataba
ya kazi na kuanza kufanya kazi baaadaye walifukuzwa kazi bila kufata
utaratibu wanatarajia kufungua kesi kesho kuishitaki serikali kwa
kitendo ilichowafanyia serikali imewafukuza kazi waajiriwa wapya wa
mahakama ,Afya, mikoani ,wilayani nk akiongea mwenyekiti msaidizi wa
wahanga hao deus mweseka ,amesema kuwa wamejipanga vya kutosha
kukabiliana na kesi hiyo ili kutafuta haki yao maana wamefukuzwa kazi
bila kuambia hata sababu ya kwanini wamefukuzwa kazi wakati wana
mikataba ya kazi na barua za kuitwa vituoni kazini amesema tangu
wafukuzwe kazi Leo huu ni mwezi wa sita wapo nyumbani amesema
anashangazwa na serikali hii kushindwa kufuta sheria na taratibu za
utumishi wa umma .
Mwenyekiti msaidizi huyo ameiomba Mahakama kuwatendea haki maana
wameitafuta haki kwa njia ya mazungumzo imeshindikana kupatikana kabisa
amesema wameonana na katibu mkuu utumishi wa umma juu ya kurudishwa
kazini lakini naye hakuwa na majibu alisema hilo swala lipo juu ya uwezo
wao lipo chini ya rais magufuli pia Waziri kairuki alisema nae kuwa
hill zoezi la watu kurudishwa kazini lipo chini ya rais na wao utumishi
wanategemea kibali ,mwenyekiti huyo alisema njia sasa ya kutafuta suruhu
juu ya swala hilo ni Mahakama pekee.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA