Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania DCP Mohamed Mpinga ameyasimamisha magari ya abiria 52 kuendelea na safari kwa kipindi cha siku 3 kutokana na mapungufu ya kiufundi na kulinda usalama wa abiria.
DCP Mpinga amesema jumla ya magari 526 yamekuwa yakiondoka katika kituo cha mabasi Ubungo, kwenda mikoani na nchi jirani katika msimu huu wa sikukuu hivyo umakini wakubaini magari yasiyokidhi vigezo unafanywa kwa uangalifu mkubwa ili kuzuia ajali.
Abiria wametakiwa kutoa taarifa iwapo dereva anaendesha kwa mwendokasi, kuhakikisha wanakuwa na tiketi ya basi husika pamoja na kukata tiketi ndani ya kituo cha mabasi Ubungo ili kuepuka matapeli, ambapo Chama cha kutetea abiria Tanzania CHAKUWA kupitia Afisa wake kituoni hapo Bwana Gervas Rutaguzinda amesema abiria wamekatiwa tiketi ya mabasi ambayo yalikishwa acha kusafirisha abiria.
Aidha Mkurugenzi wa sheria wa Mabalozi wa usalama barabarani RSA Bi. Marlin Komba amesema wamekuwa wakishugulikia kero mbalimbali za abiria kituoni hapo pamoja na kuzichukulia hatua kampuni mbalimbali zinazokatisha tiketi za magari kwa magari ambayo hayapo.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA