Ndege sawa na iliyoanguka mwaka 1972
Vesna Vulovic, mhudumu wa ndege ambaye alinusurika kifo alipoanguka kutoka ndani ya ndege iliyokuwa angani urefu wa futi 33,000 au mita 10,000 ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 66.
Kituo cha runinga cha taifa nyumbani kwa Vulovic nchini Serbia, kinasema kuwa, alipatikana akiwa amekufa nyumbani kwake mjini Belgrade.
Vulovic alikuwa akifanya kazi na shirika la ndege la Yugoslavia tarehe 26 mwezi Janauari mwaka 1972, wakati bomu lililipuka na kuangusha ndege kwenye milima ya Czechoslovakia.
Abiria wote 27 na wahudumu wa ndege waliangamia kwenye ajali hiyo.Kulingana na wachunguzi, Vulovic alikwama kwenye kigari cha chakula kwenye mkia wa ndege wakati ilianguka ardhini.Sehemu hiyo ya mkia wa ndege ilianguka eneo lenye miti mingi hali iliyookoa maisha yake.
Aliokolewa na mwanamume mmoja aliyekuwa eneo hilo baada ya kumsikia akilia gizani.
Babda ya kuwasili hospitalini alipoteza fahamu kwa siku 10 na pia alikuwa na majeraha mabaya.
Ajali jiyo ilimwezesha mhudumu huyo kuandikwa kwenye kitabu cha kumbukumbu cha Guinness Book of Records mwaka 1985 kama mtu aliyeanguka umbali mkubwa zaidi na kunusurika bila kutumia mwavuli.BBC
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA