Rapper huyo amekiambia kipindi cha Dj Shows cha Radio One kuwa anajaribu kumsaidia Chid lakini akishindwa basi haitokuwa bahati yake.
“Nadhani tuwaombee watu mabaya tuwaombee kwa mazuri arudi kwenye amani kama ilivyo kwa kila binadamu anayeishi tuombe heri. Chid na yeye anahitaji sana msaada. Unajua kitu amabacho mimi nimekigundua tusiwe na tabia kwamba mtu anapopotea au tunapompoteza duniani kabisa hayupo ndio tunaanza kumsifia kuwa alikuwa mkali,” amesema Nay.
“Mimi nataka kujaribu, nataka kuthubutu nikishindwa basi lakini namuomba Mungu iwe vile ninavyofikiria. Lakini sidhani kama ni kitu ambacho nakifikiria sana ila napenda kuona siku moja Chid anarudi katika hali yake. Nimekutana naye mara mbili na nimekaa naye tumezungumza nadhani anahitaji msaada sana, tena sana kwa hali na mali hasa watanzania wamuombee Chid anahitaji msaada,” ameongeza.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA