Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema kitendo cha kumtoa
Cristiano Ronaldo kwenye mchezo wa jana dhidi ya Levante dakika ya 82
haikuwa kwasababu ya kumpumzisha.
''Kumtoa Ronaldo lilikuwa ni suala la kiufundi wala si kumpumzisha
kwaajili ya mchezo dhidi ya PSG kama inavyodaiwa, tulikuwa tunaongoza
kwa 2-1 na hatukuweza kuongeza bao licha ya kushambulia, hivyo tulitaka
kuingiza kiungo Marco Asensio ili tumiliki mpira'', amesema.
Zidane amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuwepo kwa malalamiko
mengi kutoka kwa mashabiki ambao wanadai kutoka kwa Ronaldo
kulisababisha Levante kushambulia na kusawazisha bao la pili dakika ya
89 na kufanya mchezo umalizike kwa sare ya 2-2.
Baada ya sare ya jana Real Madrid imesalia katika nafasi ya nne ikiwa na
alama 39 huku vinara Barcelona wakiwa na alama 57 kileleni.
0 Maoni
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA